AMANI YETU TUSIIVURUGE WATANZANIA

AMANI  YETU TUSIIVURUGE  WATANZANIA

POLISI JAMII NA ULINZI SHIRIKISHI AMANI NA UTULIVU VITATAWALA DAIMA TANZANIA

Monday, October 22, 2012

MAC ,ELITE COMPUTERS (T) LIMITED NI WAUZAJI NA MAFUNDI WA MAC TANZANIA NZIMA


Elite Computers (T) Limited 
Tanzania's Leanding Apple Reseller 
East Upanga  +255716642988
Sea Cliff Village +255763277 001
Habrobour View Towers +0255 783 056 133

 Mwanza Tel; 2150663 
Email .sales@elitetz.net
Fax 2152973
P.O.BOX 38263 Dar es Salaam Tanzania

Friday, August 24, 2012

SENSA YA WATU NA MAKAZI KUANZA LEO SAA 6 USIKU ITADUMU SIKU SABA JIANDAE KUHESABIWAMkuu wa mkoa wa Iringa Dr.Christine Ishengoma amewataka wananchi wa mkoa wa Iringa kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi ,zoezi litakaloanza usiku wa leo jumamosi ya Agost 25 kuamkia Agost 26 mwaka huu.

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalum na mtandao huu wa www.francis Godwin.blogspot.com kuhusiana na maandalizi ya zoezi hilo kwa mkoa wa Iringa.

Amesema kuwa hadi sasa mandalizi ya zoezi la sensa kwa mkoa wa Iringa yamefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90 na kuwa wananchi wote wanapaswa kutoa ushirikiano wao kwa makarani wa sensa watakaofika katika maeneo yao.

Dr.Ishengoma amesema kuwa zoezi hilo la Sensa ni kwa watanzania wote hivyo lazima makundi yote kujitokeza kuhesabiwa bila kuwabagua wazee,walemavu katika kuhesabiwa .

Ametaka wakuu wa kaya kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa Sensa na kuwa mkuu wa kaya atakayewazuia makarani wa sensa kuifanya kazi hiyo hatua kali atachukuliwa .

Habari hii kwa udhamini wa Tanzania Unique Tours Iringa

ANZANIA UNIQUE TOURS NI UHAKIKA KWA SAFARI ZA MAENEO YA VIVUTIO NCHINI

Magari ya kisasa yanayotumika kusafirisha watalii katika maeneo ya vivutio hapa nchini kutoka kampuni ya Tanzania Unique Tours
Hapa ni safari salama na Tanzania Unique Tours
Watalii wakiwa wamepanga foleni ofisi za Tanzania Unique Tours kwa ajili ya kukodi

ofisi zetu zipo nyumba ya jengo la Highlands Hall(Behind Highland Hall) jirani na posta ya mkoa wa Iringa ,Manispaa ya Iringa ,P.O.Box.384 Iringa Mob.+255 656 187139/0759248284
Tanzania Unique Tours
Service;
> Mountain Climbing /Trekking
>To Organize safari& Tours
> Hotels Accommodation .
CONTACT
Tell+225(0)02702425
Cell;07155961433
Email Info2@tanzaniauniquetours.com
website.www.tanzaniauniquetours.com
BOFYA HAPA KWA TAARIFA SASA KWA TAARIFA ZAIDI

Thursday, August 2, 2012

Tamko la HakiElimu kuhusu Mgomo wa Walimu Tanzania, Agosti 2012

Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia (kulia) akitoa tamko kwa wanahabari kuhusiana na mgomo mchana huu jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kulia ni Meneja wa Kitengo cha Habari na Ushauri, HakiElimu. (Picha na Joachim Mushi)

CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT) kiliitisha mgomo kwa walimu wote nchini kuanzia Jumatatu tarehe 30 Julai 2012 mpaka kitakapowajulisha vinginevyo. CWT kinaona mgomo ndio njia sahihi itakayoishinikiza Serikali kutekeleza madai ya walimu na kuwaboreshea mazingira ya kazi walimu. Mgomo huu leo unafikisha siku ya nne mfululizo.
HakiElimu inatambua kuwa walimu wamekuwa na mgomo baridi kwa muda mrefu sasa. Utafiti uliofanywa na HakiElimu mwaka jana ulibaini kuwa asilimia 40.6 tu ya walimu katika sampuli ya utafiti ndio walioonesha nia ya kuendelea kuwa walimu, wakisema mazingira magumu na maslahi duni ndio sababu kubwa za kuwavunja moyo. Uthibitisho mwingine wa kuwepo kwa mgomo baridi unatokana na kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya Taifa. Kwa mfano katika shule za msingi, takribani nusu ya wanafunzi wamekuwa hawafaulu kwa miaka 3 sasa; huku mwaka 2011 pekee ukiwa na asilimia 46.5 ya watahiniwa waliofeli mitihani yao ya darasa la saba; na kwa sekondari wanafunzi takribani asilimia 90 walipata daraja la nne na sifuri.
Hali hii pia inadhihirishwa zaidi na uwepo wa wanafunzi zaidi ya 5,000 mwaka huu nchini walioandikishwa kujiunga na masomo ya sekondari kutokujua kusoma na kuandika. Pia ripoti ya utafiti uliofanywa kwa niaba ya African Economic Research Consortium na Benki ya Dunia mwaka 2011 inaonesha kwamba walimu wa shule za msingi Tanzania wanafundisha kwa wastani wa masaa mawili na dakika nne tu kwa siku; kati ya masaa 5 na dakika 12 yaliyo katika ratiba ya siku moja.
Mambo haya yote yanadhihirisha kuwa mgomo baridi wa walimu umeendelea kuwepo, na kuwaathiri zaidi wanafunzi. Wanafunzi hawawezi kujifunza bila walimu; na walimu bila kufundisha kwa moyo, wanafunzi hawawezi kujifunza kwa ukamilifu.
Ni dhahiri kuwa mgomo huu wa walimu umekuwa na madhara makubwa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Wanafunzi wanakosa masomo. Hii itachelewesha kumaliza ‘mihtasari’ (syllabuses) ya kufundishia, na kuwaumiza zaidi wale watakaofanya mitihani yao ya Taifa mwaka huu. Usalama wa wanafunzi uko hatarini, hasa wanapoamua kwenda shuleni kwa kuhisi kuwa huenda walimu wao watafundisha kwa siku hiyo. Ni hatari sana wanafunzi kuwepo shuleni bila walimu. Wanakosa mwongozo wa walimu, na kuishia kurandaranda maeneo ya shule, ama mitaani.
Pia mgomo huu unajenga mtazamo hasi wa jamii kuhusu kazi ya ualimu. Wanafunzi na wazazi wao wanaendelea kutengeneza tafsiri kuwa kazi ya ualimu ni duni sana, na baadhi ya kauli za serikali kuhusu mgomo huu haziijengei hadhi kazi hii adhimu. HakiElimu pia inaamini kuwa mgomo huu utaligharimu Taifa kwa namna mbalimbali. Kwa kadri unavyochelewa kwisha, unaweza kubadilisha mihula masomo, ratiba za mitihani ya Taifa, na hata sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi huu inaweza kuingia dosari. Wazazi wa wanafunzi hasa walio shule za bweni wanatafakari hatma ya watoto wao. Je, wawarudishe nyumbani au waendelee kukaa shuleni?

Baadhi ya wanahabari waliusikiliza uongozi wa HakiElimu

Baada ya kuyatafakari haya, HakiElimu inapendekeza yafuatayo:
1. Kila mwanafunzi ana haki ya kujifunza na kuelimishwa. Hivyo basi, Serikali na Chama Cha Walimu Tanzania wanapaswa kufikia makubaliano haraka kadri inavyowezekana, kwa kuwa waathirika wakubwa wa mgomo sio wao wenyewe, ni wanafunzi.
2. Mgomo huu ushughulikiwe na uishe kabisa. Usiishie kuwaona walimu wamerejea kufundisha, huku wakiwa na kinyongo. Hii italeta mazingira ya kuendeleza mgomo baridi; na madhara yake ni makubwa zaidi.
3. HakiElimu inawakumbusha walimu kuwajibika. Wadai haki zao, huku wakitimiza wajibu wao wa kufundisha na kuendeleza elimu yetu. Wafundishe kwa bidii bila kinyongo, kwa kuwa wasipowajibika watakuwa wanawaumiza wanafunzi na jamii kwa ujumla. Mgogoro uliopo ni baina yao na Serikali, na si wanafunzi.
4. Kusema serikali haina uwezo wa kuboresha maslahi na mazingira ya kazi ya watumishi wake; haileti unafuu wa maisha kwa watumishi wa umma. Gharama za maisha zinazidi kupanda, na mfumuko wa bei nao unawaumiza watumishi kila siku. Hivyo, Serikali itafute vyanzo mbadala vya mapato. Isitoshe, serikali iweke malengo, mipango na mikakati ya kuboresha elimu na mazingira ya kufundishia kwa kuwa ndio njia muafaka na ya haraka ya kuiletea nchi maendeleo.
5. HakiElimu inasisitiza kwamba nchi itafanikiwa kuboresha elimu endapo tu itawekeza kwa walimu kwa kuboresha mazingira ya kazi, maslahi ya walimu, kuwashirikisha walimu katika maamuzi kuhusu masuala ya elimu na kuwapa walimu mafunzo kazini. Elimu bora haiwezi kuletwa na walimu walio hoi!
6. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litenge muda kujadili suala hili kwa kina na kuishauri serikali, hasa kuhusu tahadhari za kuchukua ili tatizo kama hili lisitokee tena. Bunge lina wajibu wa kuishauri na kuisimamia Serikali kuhusu sera, utendaji na usimamizi wa elimu nchini. Inasikitisha kwamba Bunge linakwepa kujadili tatizo hili kwa maelezo kwamba liko mahakamani. Tunaamini kwamba mahakama italiangalia suala hili na kutenda haki, lakini wajibu wa Bunge uko pale pale.
7. Viongozi wa Serikali wasiwabeze walimu; kwa kufanya hivyo wanawakatisha tamaa. Hata kama baadhi ya walimu hawakusoma kwa miaka mingi kama ilivyo kwa fani nyingine, wana umuhimu mkubwa sana. Ndio wanaowaandaa watanzania wa leo na kesho kimtazamo na kimaarifa. Hivyo, kudai kuboreshewa mazingira ya kazi ni haki yao; na Serikali inaweza kutimiza wajibu wake kwa kuwasikiliza na kushauriana nao bila ubabe na kejeli.
8. Serikali ijijengee utaratibu wa kuboresha mazingira ya watumishi wake, na si kusubiri kwenda mahakamani kuzuia watumishi kugoma. Watumishi wa umma watafanya kazi kwa ari endapo tu wameridhika na mazingira ya kazi na maslahi yao; na si kwa kutumia uamuzi wa mahakama peke yake.

HakiElimu ni shirika la jamii linalowawezesha wananchi kubadilisha elimu, ndani na nje ya shule; kuathiri utungaji na utekelezaji madhubuti wa sera; kuchochea majadiliano ya umma na mabadiliko ya kijamii yenye ubunifu; kufanya utafiti, uchambuzi na uhamasishaji wa sera, na kushirikiana na wabia ili kuendeleza ushiriki, uwajibikaji, uwazi na haki za jamii. Shirika linataka kuona Tanzania inaongeza uwazi, haki na demokrasia kwa kuwapa watu wote fursa ya kupata elimu inayochochea usawa,ubunifu na fikra tunduizi.

Elizabeth Missokia Mkurugenzi Mtendaji

Short URL: http://www.thehabari.com/

Saturday, June 16, 2012

MHARIRI WA GAZETI LA JAMBOLEO WILLY EDWARD AMEFARIKI DUNIA GAFLA


Habari za kusikitisha zilizotua katika mtandao huu wa asubuhi hii kutoka mkoani Morogoro zinaeleza kuwa aliyekuwa mhariri wa habari wa gazeti la Jamboleo Willy Edward (pichani) amefariki dunia .

Willy Edward alikuwepo mkoani Morogoro katika mafunzo ya siku moja pamoja na wanahabari wengine na kuwa inadaiwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pumu kwa muda mrefu .

mpenzi mdau wa mtandao huu habari zaidi juu ya kifo cha Willy Edward utaendelea kuzipata zaidi katika mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com

Sote tulimpenda sana Willy Edward ila Mungu kampenda zaidi yetu hivyo jina lake Mungu na lihimidiwe zaidi .

Amina

Friday, May 4, 2012

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA , LUKUVI APETA , MAKALA ,Dkt MAHENGE ,DKT MGIWA AULA

Rais Dkt Jakaya Kikwete
Mbunge wa jimbo la Ismani Iringa Wiliam Lukuvi ambaye ameachwa tena katika nafasi yake ya uwaziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge
mbunge wa jimbo la Makete mkoa mpya wa Njombe Eng. Dr. Binilith Mahenge, (kushoto) ambaye ameteuliwa kuwa naibu waziri wa maji akiwa na mkuu wa wilaya Dkt Norman Sigalla
Mbunge wa jimbo la Kalenga Dkt Wiliam Mgimwa aliyeteuliwa kuwa waziri wa fedha na uchumi leo ,hapa akisaini hundi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari Lyandembela jimboni kwake
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

MAWAZIRI

1. OFISI YA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)

Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)

Ndugu George Mkuchika, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)

Ndugu Celina Kombani, Mb.,

2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)

Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)

Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,

3. OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)

Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)

Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,

4. WIZARA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

Waziri wa Ujenzi

Dr. John P. Magufuli, Mb.,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,

Waziri wa Katiba na Sheria

Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,

waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Dr. David M. David, Mb.,

Waziri wa Kazi na Ajira

Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,

Waziri wa Maji

Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum

Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

Eng. Christopher Chiza, Mb.,

Waziri wa Uchukuzi

Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

Waziri wa Maliasili na Utalii

Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara

Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha

Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini

Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,

5. NAIBU MAWAZIRI

OFISI YA RAIS

HAKUNA NAIBU WAZIRI

OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais

Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,

7. OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,

8. WIZARA MBALIMBALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira

Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

Ndugu Adam Malima, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,

Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

Naibu Waziri wa Ujenzi

Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,

Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini

Ndugu George Simbachawene, Mb.,

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi

Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji

Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini

Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria

Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha

Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha

Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

4 Mei, 2012

Monday, November 28, 2011

MAHAFALI YA 15 CHUO CHA UFUNDI STADI VETA IRINGA NA CHANGAMOTO ZAKE

MAMLAKA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI

TAARIFA FUPI YA CHUO CHA VETA IRINGA

CHUO CHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI NA HUDUMA IRINGA

Mheshimiwa mgeni rasmi: Mjumbe wa bodi ya VETA Kanda ya Nyanda za juu

Mkurugenzi wa VETA Kanda ya nyanda za juu,
Wakuu wa taasisi mbalimbali,
Waandishi wa habari,
Wageni mbalimbali walio pamoja nasi,
Wafanyakazi wenzangu wote wa VETA
Wahitimu wote,
wanafunzi wote wanaoendelea na mafunzo,
mabibi na mabwana,

Awali ya yote nakushukuru sana wewe binafsi kwa kukubali kushiriki nasi katika Mahafali haya ya 15 ya Chuo chetu.
Aidha niwapongeze kwa dhati kabisa wageni wetu wote kuja kushiriki nasi katika kuwapongeza na hatimaye kuwatunuku Vyeti Wanachuo wetu ambao wamehitimu mafunzo yao.

Mheshimiwa mgeni rasmi,

Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Iringa kinamilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Tanzania (VETA).

Chuo hiki kilifunguliwa rasmi na kuanza utoaji wa Mafunzo mnamo January 1997.

1.Mafunzo yotolewayo
Mheshimiwa mgeni rasmi,

Chuo chetu kinatoa mafunzo ya muda mrefu na mafunzo ya muda mfupi.
· Mafunzo ya muda mrefu yatolewayo hadi sasa ni ya fani mbalimbali kumi na moja (11) kama ifuatavyo:-

1. Umeme wa majumbani
2. Uhazili
3. Useremala
4. Uashi
5. Utengenezaji wa Magari
6. Uungaji vyuma
7. Ukerezaji na Uchongaji Vyuma
8. Upakaji rangi Majengo na Maandishi
9. Ufundi bomba
10. Ushonaji nguo
11. Utayarishaji wa Vyakula

Mafunzo ya muda mfupi
Mheshimiwa mgeni rasmi,

Sambamba na Mafunzo ya muda mrefu Chuo kinatoa pia Mafunzo ya muda mfupi kulingana na mahitaji ya mteja. Zifuatazo ni kozi ambazo Chuo kimeendelea kuzitoa:-
· Udereva
· Kompyuta
· Uhazili

Mheshimiwa Mgeni rasmi,
Chuo kina jumla ya wanafunzi 303 hadi tarehe ya leo (Wasichana 79 Wavulana 224) wasichana asilimia 26.1 Wavulana asilimia 73.9


NA.
FANI
L -I MWAKA WA 1
L-I MWAKA WA 2
L - 2

WAS
WAV
JUML
WAS
WAV
JUMLA
WAS
WAV
JUMLA
JUMLA KUU
1.
USEREMALA0
09
09
0
16
16
25
2.
UMEME01
20
21
0
19
19
40
3.
UHAZILI
22
02
24
16
0
1640
4.
BOMBA02
13
15
0
07
07
22
5.
UCHONGAJI
V YUMA
01
17
18
0
12
1230
6.
UUNGAJI VYUMA
01
18
19
0
15
1534
7.
UASHI0
08
08
0
15
15
23
8.
UTAYARISHAJI CHAKULA*
16
02
18
-
-
-
-
-
-
18
9.
RANGI NA MAPAMBO
02
11
13
05
08
13
-
-
-
26
10.
USHONAJI NGUO09
02
11
04
0
04
15
11.
MAGARI
0
18
18
0
12
1230
JUMLA
42
68
110
33
99
132
04
57
61
303
2.WAHITIMU
Mheshimiwa mgeni rasmi
Katika Mahafali ya leo tunao Vijana 79 (wasichana 20 sawa na asilimia 25.3 na Wavulana 59 sawa na asilimia 74.7
NA.
FANI
WASICHANA
WAVULANA
JUMLA
1.
Uzalishaji Chakula
16
02
18
2
umeme
0
19
19
3
Ushonaji Nguo
04
0
04
4.
Useremala
0
16
16
5.
Bomba
0
07
07
6.
Uashi
0
15
15

Jumla
20
59
79


3. Mafanikio
Mheshimiwa mgeni rasmi,
Katika kutekeleza majukumu yake na malengo mbalimbali Chuo kimepata mafanikio yafuatayo:-
3.1 Kozi fupi
Mwaka huu wa 2011 Chuo kinategemea kutoa jumla ya wahitimu wa kozi fupi zaidi ya 400).
3.2 Kujitangaza
Kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari, Chuo kimekuwa kikiyatangaza mafunzo yake na huduma mbalimbali zinazotolewa hapa,hatimaye kupata mwitikio unaostahili.
3.3 Mafunzo ya Watumishi
Waalimu 05 wamekwenda kuchukua Mafunzo mbalimbali ya muda mrefu. Na Mkutubi 01.
3.4 Huduma mbalimbali:-
Chuo kimeendela kutoa huduma mbalimbali kama
Kantini inavyotoa huduma ya vyakula na vinywaji kwa wateja mbalimbali.
Hostel ya wageni yenye vyumba 20
Kumbi mbalimbali za mikutano na sherehe
3.5 Chuo kimeweza kukamilisha hadi sasa majukumu yake kulingana na mpango kazi.

3.6 Kwa kushirikina na Wanachuo, kazi mbalimbali zilifanyika kwenye karakana, kazi za nje, michezo na shughuli za mazingira zimetekelezwa na zinaendelea kutekelezwa ipasavyo.

3.7 Chuo kimeendelea kushirikina na taasisi mbalimbali ndani na nje ya Iringa katika kuboresha utendaji kazi.


3.8 Mipango yetu mwakani:
Mategemeo ya mwakani ni kupanuwa fani ya utayarishaji wa vyakula kwa kuanzisha idara za
· Front office.
· House keeping.
· Food bevarage and selling.
3.9 Mipango ya baadaye.
Kwa vile eneo la chuo chetu ni Kidogo pengine kuliko vyuo vyote vya VETA Tanzania, chuo kina mpango wa kujenga mabweni eneo la Kitwiru ili kuongeza idadi ya Wanafunzi.

4. Changamoto
Mheshimiwa mgeni rasmi,
Kila penye mafanikio na changamoto zinakuwepo, kwa mfano:-

4.1 Mafunzo kwa vitendo (Field training), ili vijana waweze kuwa mahiri katika fani zao, mafunzo kwa vitendo ni muhimu sana.
Pamoja na jitihada za Chuo za kutafuta sehemu mbalimbali za kufanyia mafunzo hayo: kumekuwepo vikwazo kadhaa kama vile, Wadau wengine kukataa kuwapokea vijana, kwa kudai gharama za mafunzo yao wanapokuwa kwenye sehemu zao.

4.2 Chuo kina uwezo wa kuchukuwa wanafunzi zaidi ya 350 lakini mabweni yaliyopo huchukuwa wanafunzi 106 tu kati ya hao wasichana ni 30 na wavulana ni 76 hivyo kusababisha waombaji wengi kutochukuliwa kujiunga na Chuo.Tumejaribu kutafuta Mabweni ya bei nafuu ndani ya Manispaa ya Iringa lakini tumeshindwa.

4.3 Michezo
Kutokana na eneo la Chuo kuwa dogo, Wanachuo wanapata matatizo ya kushiriki kikamilifu kwenye michezo mbalimbali baada ya masomo.Hata hivyo tunawashukuru jirani zetu wa shule ya Msingi Mlandege ambao wamekuwa wakitusaidia kutatua tatizo hili.

4.4 Maji
Chuo kimekuwa kikikabilina na tatizo la kukatika maji kutoka vyanzo vya JR IRUWASA na hivyo kuathiri mafunzo na utoaji wa huduma nyinginezo za hapa Chuoni.

4.5 Umeme
Chuo kama sehemu ya jamii kimeendelea kupambana na adha ya kukatika mara kwa mara kwa umeme ambao ni nishati muhimu katika kutekeleza majukumu yake kitendo ambacho suluhisho lake ni kuwa na jenereta lenye uwezo mkubwa.
5. Hitimisho

Mheshimiwa mgeni rasmi,
Ninachukua fursa hii, kuwapongeza sana Wanachuo kwa juhudi, usikivu wao na nidhamu katika ufuatiliaji wa mafunzo yao na hivyo kuleta mafanikio makubwa kwao na kwa Chuo chetu.

Tunaowaomba waendelee na ari hiyo ili waweze kuboresha maisha yao huko waendako.

Aidha, tunawaomba wahitimu wetu wawe mabalozi wetu wazuri kuwashauri Vijana wenzao kujiunga na Vyuo mbalimbali vya Mafunzo ya ufundi Stadi, kwani Ufundi ni jibu la haraka katika harakati za kupambana na kutokomeza umaskini hasa pale ambapo kijana ataajiriwa au kujiajiri.

Ahsanteni sana.

Monday, September 13, 2010

BARABARA YA MAFINGA-KIBAO NI BARABARA MBOVU INYOCHANGIA UCHUMI WA TAIFA


Barabara hii ya Kibao -Mafinga ni barabara inayoiwezesha wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kuwa mbele katika makusanyo ya mapato na ni moja kati ya barabara zinazochangia kukuu kwa uchumi wa Taifa la Tanzania kutokana na ukubwa wa kiwanda cha karatasi Mgogolo ambacho ni kiwanda kimojawapo kikubwa kwa Afraka ila barabara yake hadi sasa haina hata chembe ya lami
Hii ni